Chinese
Fahamu jinsi ya kuandaa shamba la chinize na vitu gani unatakiwa kufahamu kuhusu chinize . Spinachi ni moja kati ya mazao ya mbogamboga inayo limwa sana nchini Tanzania na asili yake ni china na ndo maaana huwa tunaiita chinese na badae likasambaa katika nchi mbalimbali ikiwemo na Tanzania. Mboga hii huwa haina msimu, hivyo mkulima anaweza kulima muda wowote ambao anataka, na hii itategemea upatikanaji wa maji wa maji kwa wingi. Kwani mboga hii huhitaji maji kwa wingi katika hatua za awali. Hali ya hewa inaoyofaa kwa kilimo hiki ni. Jotolidi; Chinese au linastawi na kukua vizuri kwenye maeneo yenye jotolidi 18 °c hadi 27° c. Unyevunyevu; chinese ni zao linalo tegemea umwagiliaji kama ambavyo nimekwisha eleza hapo awali hivyo linaitaji maji mengi wakati wa ukuaji. Udongo; chinese cabbage linakua vizuri kwenye udongo wa kichanga na wenye unyevunyevu wa kutosha PH; 5.5 hadi 7.6 Namna ya kuandaa shamba. Udongo unatakiwa utifuliwe vizuri kabla ya kupa...