Chinese

 Fahamu jinsi ya kuandaa shamba la chinize na vitu gani unatakiwa kufahamu kuhusu  chinize .



Spinachi ni moja kati ya mazao ya mbogamboga inayo limwa sana nchini Tanzania na asili yake ni china na ndo maaana huwa tunaiita chinese na badae likasambaa katika nchi mbalimbali ikiwemo na Tanzania.

Mboga hii huwa haina msimu, hivyo mkulima anaweza kulima muda wowote ambao anataka, na hii itategemea upatikanaji wa maji wa maji kwa wingi. Kwani mboga hii huhitaji maji kwa wingi katika hatua za awali.

Hali ya hewa inaoyofaa kwa kilimo hiki ni.
Jotolidi; Chinese au  linastawi na kukua vizuri kwenye maeneo yenye jotolidi 18 °c hadi 27° c.

Unyevunyevu; chinese  ni zao linalo tegemea umwagiliaji kama ambavyo nimekwisha eleza hapo awali hivyo linaitaji maji mengi wakati wa ukuaji.

Udongo; chinese cabbage linakua vizuri kwenye udongo wa kichanga na wenye unyevunyevu wa kutosha PH; 5.5 hadi 7.6

Namna ya kuandaa shamba.
Udongo unatakiwa utifuliwe vizuri kabla ya kupanda unaweza kutumia jembe la mkono au machaku na chisel na andaa shamba wiki 6 kabla ya kupanda.

Uandaaji wa kitalu.
Kitalu kinatakiwa kiwe na upana wa mita 1.5yani sentimita 115 na urefu wa mita 5.5yani sentimita 550 Kitalu kitifuliwe vizuri na kiwe na kingo ili kuzuia maji kutoka nje ya kitalu. kisha panda mbegu kwenye kitalu kwa sm 10hadi 15 mstari hadi msitari na panda mbegu sm 2 kati ya mbegu na mbegu na fukia sm 1 hadi 2.

Kupanda
Kwa kupanda moja kwa moja chimba udongo sm 2 hadi 3 kwa kutumia jembe la mkono na panda nafasi ya 30 mstari hadi mstari na 30 mbegu hadi mbegu na fukia sm1 hadi 2.
Na kwakupandikiza hamisha miche inapo fikia urefu was sm 5 na chagua miche yenye afya na isiwe na magonjwa.

Mbolea.
Kama unatumia mbolea ya ng’ombe, kuku tumia ndoo katika kila kitalu chenye mita 5.5
Na pia weka mbolea ya kukuzia UREA gram 50 kwa kila kitalu chenye mita 5 pale mmea unapofikia majani matano.

Palizi
Tumia jembe la mkono kupalilia magugu pale yanapo jitokeza.

Magonjwa na wadudu waharibifu
Pale utakapohisi majani ya mboga hizi yameanza kubadikika, ikiwa ni ishara ya kushambuliwa na wadudu, tafadhari unashauriwa uweze kutumia chemicali za kuua wadudu kama vile ninja, supercorn, wilcron na perfecron na pia hakikisha kila wakati unakumbuka kuondoa  magugu pamoja na mimea yenye wadudu na pia weka shamba safi wakati.

Lakini kama utatokea ugonjwa wa Kuoza kwa mizizi unachotakiwa kufanya kuondoa mazao yaliyo athilika na ugonjwa huo.

Kuvuna
Chinese ukomaa baada ya miezi 2 hadi 4 inategemea na aina mbegu uliyopanda, au muda mwingine hutegemea na hali ya hewa pia.

Linki inayo onesha jinsi kuvuna chinize
https://youtu.be/3bj5ZMj2jPg

Video inao nesha jinsi ya kuvuna chinize


Picha inaonesha chinize iliyo komaa


Kumbuka;
Wakati wa kuvuna unang’oa kwa mkono au unaweza kutumia kisu kukata kuanzia chini kabisa ya shina ili kuruhusu majani mengine ya mboga kukomaa.


Audio ya jinsi ya kuvuna mchicha


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog